MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA KILIMO YATARAJIWA.

Na

 Egidia Vedasto,

Arusha.

Wadau wa sekta ya kilimo, ufugaji pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali za mikoa ya kanda ya kaskazini wamekutana jijini Arusha kujadili namna ya kumnyanyua mkulima mdogo, kutafuta masoko na kujenga maghala ili kuhakikisha mazao yanayovunwa hayaharibiki.

Akizungumza katika mkutano huo , februari 10,2026,mkuu wa mkoa Tanga Balozi Batrida Burhani amesema watahakikisha uhamasishaji, ukuzaji na uendelezaji wa shoroba za kilimo. Amefafanua kuwa kipindi tunachoelekea nchi itapokea wageni wengi hivyo ni wakati wa kujipanga sawasawa.

Aidha amesisitiza wanawake na vijana kushirikishwa kwa upana, kushauriwa kulima kilimo chenye soko ikiwemo mbogamboga na matunda.

"Sekta ya kilimo ni mtambuka, inagusa sekta nyingine nyingi ikiwemo biashara, viwanda ardhi na nyinginezo, si hivyo tu bali inaajiri watu wengi. Nawaomba sana wataalamu wa AGCOT na ATO kusambaza uzoefu wenu kwa wadau wote wa kilimo ili kufikia malengo ifikapo 2030" amesema Balozi Batilda Burihani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Agriculture Transformation Officer (ATO) Elizabeth Missokia amesema lengo la mkakati huo ni kuunganisha wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi, kuimarisha sekta binafsi, kuweka mfumo wa tathmini na kulima mazao ya kusindika ifikapo mwaka 2030.

"Katika mageuzi haya tutazingatia ujumuishi wa wanawake na vijana, takribani kwa miaka 10 tumekukuwa na shoroba 1 ambayo imeleta mageuzi kwa asilimia 65 ya chakula" amesema Elizabeth.

Katika namna hiyo hiyo Mkuu wa wilaya Arusha Joseph Mkude akimwakilisha mkuu wa mkoa Arusha CPA. Amos Makalla amesema kuwa mageuzi hayo yakifanikiwa yataondoa umaskini kwa wakulima wadogo.

"Tumekuwa tukishuhudia mazao yakiozea shambani kwa sababu ya kukosa masoko, naamini huu utakuwa mwarobaini kwa wakulima wadogo ambao ndio wenye idadi kubwa nchini" amefafanua  Mkude.







 

0/Post a Comment/Comments