Neema kwa Watumishi Ngorongoro: Milioni 500 Zatolewa, Tahadhari Dhidi ya Mikopo Hatari.

Na 

Mwandishi wetu,

Arusha.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Murtallah Sadick Mbilu, amesema serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuwasaidia watumishi wa umma katika wilaya hiyo.

Amesema kuwa fedha hizo zinalenga kuwawezesha watumishi wa kada mbalimbali kujikwamua kiuchumi, hasa kwa kuepuka mikopo ya riba kubwa maarufu kama “kausha damu”.

Akizungumza Aprili 2,2026,katika mahojiano maalumu na Yawhe FM, Mbilu amesema ni muhimu kwa watumishi kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili iweze kuleta manufaa binafsi na kwa taasisi.

Aidha, amesema mkopo huo pia utasaidia kupunguza changamoto ya usafiri kwa watumishi wengi wanaofanya kazi katika maeneo ya mbali ndani ya wilaya hiyo.

Pia Mbilu amesema kuwa utoaji wa mikopo hiyo umewekwa katika mfumo rasmi unaowezesha kila mtumishi kuomba kwa uwazi, hatua ambayo inalenga kuondoa mgongano wa maslahi.

Aidha ameongeza kuwa kupitia mpango huo, halmashauri inatarajia kuongeza ufanisi wa watumishi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
 

0/Post a Comment/Comments