BASI TATU ZA LOLIONDO COACH ZANUNULIWA KWA MPIGO.



Na, Egidia Vedasto,

Arusha.

Kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya Loliondo coach inayopatikana Jijini Arusha yamewahakikishia abiria wake usalama wa kutosha pamoja na huduma bora kila wakati wawapo safarini.

Hayo yamesemwa na  Chilia kimambo mkurugenzi mtendaji was mabasi ya Loliondo Coach    baada ya kununuliwa kwa mkupuo mabasi mapya matatu ishara hiyo ikionyesha hatua kubwa ya kibiashara na uhakika wa usafiri kwa watumiaji wake.

Aidha amewaomba wateja kuendelea kuiamini kampuni hiyo na kuwaahidi huduma bora daima.

"Nawashukuru sana wateja wetu, nakiri kuwa mafanikio haya yametokana na upendo na utayari wenu kwa kutumia mabasi yetu kwa miaka mingi" amesema Chilia.

Mmoja wa wateja Lucy Godfrey anayetumia mabasi hayo mara nyingi kutoka Arusha kwenda Musoma, amepongeza kampuni hiyo kwa hatua kubwa ya mafanikio.

Amesema kuwa huduma zao ni nzuri na wana lugha nzuri wanapowasiliana na wateja wao.

Kampuni ya mabasi ya Loliondo Coach ni kongwe na inayoaminika na wengi. Hufanya safari zake kuanzia Moshi kwenda Mwanza hadi Musoma.





0/Post a Comment/Comments