Na
Bora Mustafa,
Arusha.
Kampuni ya mama G Cosmetics imetangaza uzinduzi wa bidhaa zake mpya zinazotengenezwa kwa viambato vya asili. Bidhaa hizi zinasaidia kutibu chunusi, miwasho, na mapunye kwenye ngozi.
Loveness Mgonja, Afisa Masoko wa kampuni hiyo, amesema bidhaa hizo zinatumia miti na mitishamba ya asili kama mwarobain, alovera, mlonge, pamoja na mafuta ya karoti, zabibu, na ubuyu.
“Tunataka Watanzania wapende bidhaa za asili ili kulinda afya yao na kuepuka kemikali mwilini,”
alisema Loveness, akihimiza wito huu kuelekea Siku ya Wanyama Porini Duniani.
Bidhaa za G Cosmetics zinapatikana Arusha Mianzini na mikoa jirani ikiwa ni pamoja na Kilimanjaro, Manyara, Babati, Morogoro, na Dar es Salaam.

Post a Comment