Arusha Yapiga Hatua: Malalamiko ya Wananchi Yapungua kutoka 50 hadi 16


Bora Mustafa,

Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Joseph Mkude, amezindua rasmi zoezi la usikilizaji wa kero za wananchi katika ngazi ya wilaya, hatua inayolenga kuimarisha uwajibikaji na utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi.

Katika uzinduzi huo , zaidi ya kero 16 zimesikilizwa, zikiwemo zinazohusu ardhi na mirathi. 

Akizungumza April 1,2026, Mhe. Mkude ameeleza kuwa idadi ya malalamiko imepungua kwa kiasi kikubwa kutoka zaidi ya kero 50 hadi kufikia 16, jambo ambalo ni matokeo ya usimamizi mzuri wa zoezi hilo katika ngazi ya kata.

 Pia Amesisitiza umuhimu wa watendaji wa serikali kuendelea kusimamia kikamilifu utatuzi wa changamoto za wananchi katika maeneo yao, ili kupunguza mlundikano wa kero katika ngazi ya wilaya.

Aidha, Mhe. Mkude amebainisha kuwa kero ambazo hazijapatiwa ufumbuzi katika ngazi za chini ndizo zinapaswa kupandishwa hadi ngazi ya wilaya kwa hatua zaidi.

Kwa Upande Mwingine , mkuu wa wilaya amesema uongozi umejipanga kuhakikisha maagizo ya Mkuu wa Mkoa yanatekelezwa, ambapo kila Mkuu wa Wilaya anatakiwa kusikiliza kero za wananchi kila Jumatano ya mwisho wa mwezi.

 pia a meongeza kuwa zoezi hilo ni sehemu muhimu ya kuimarisha mawasiliano kati ya serikali na wananchi, pamoja na kuhakikisha changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.




0/Post a Comment/Comments