CRDB Yaongeza Kasi ya Huduma za Kidijitali Kuwafikia Wananchi


Na

 Mwandishi wetu,

Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Joseph Mkude ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuendelea kuimarisha uwekezaji katika teknolojia za kidijitali zinazolenga kuongeza ubora na ufanisi wa huduma za kifedha kwa wananchi wa mijini na vijijini.

Akizungumza  leo june 15,2026 jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa kampeni ya CRDB Bonge la Wakala, amesema matumizi ya mifumo ya kidijitali yana mchango mkubwa katika kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Ameeleza kuwa hatua hiyo inaendana na mkakati wa Serikali wa kuimarisha uchumi wa kidijitali nchini, huku akiitaka benki hiyo kuendelea kuja na huduma bunifu zitakazowezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za kifedha kwa urahisi, usalama na kwa wakati.

Aidha MKude amepongeza maendeleo yaliyofikiwa ambapo takribani asilimia 98 ya huduma za benki kwa sasa zinafanyika kupitia mifumo ya kidijitali, hali inayorahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza idadi ya wananchi wanaonufaika na sekta ya fedha.

"Uwekezaji huo unaunga mkono juhudi za kitaifa za kujenga uchumi shirikishi unaotumia teknolojia,  nasisitiza benki hiyo kuendelea kupanua huduma zake na kuongeza uwekezaji katika ubunifu wa kidijitali" Amesema.

Kwa upande wake, Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini, Emmanuel Kafui amesema kupitia kampeni ya CRDB Bonge la Wakala, wateja watakaotumia huduma mbalimbali za kifedha watapata nafasi ya kujishindia fedha taslimu na zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya huduma hizo.

Naye mmoja wa Mawakala wa benki hiyo, Juliana Abraham amesema wako tayari kuendelea kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali ya Arusha kwa kutoa elimu ya matumizi ya huduma za kifedha na kuwahamasisha kutumia huduma za benki kupitia mawakala waliopo karibu nao. 

Uzinduzi huo umefanyika chini ya kauli mbiu “Bonge la Wakala Simu Bank Kimpango Wako.





0/Post a Comment/Comments