JAMII YATAKIWA KUUNGANA KUPAMBANA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA NA UKATILI WA KIJINSIA


 

Na,

Jennifer Lazaro,

Arusha.

Jamii imetakiwa kuimarisha juhudi za pamoja katika kupambana na matumizi ya pombe, dawa za kulevya na tumbaku pamoja na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

 Akizungumza Leo Novemba 17,2026 kwenye warsha iliyowakutanisha waandishi wa habari mkoani ARUSHA, Glory Vincent, Afisa Mradi na Mwezeshaji kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Blue Cross Society Tanzania, amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya vilevi na vitendo vya ukatili wa kijinsia, hivyo elimu kwa jamii ni muhimu katika kupunguza changamoto hizo.

Amesema vijana wenye umri wa miaka 12 hadi 16 ni miongoni mwa makundi yanayoanza kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya, hivyo kuwataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao, kuwapatia malezi bora na kufuatilia mienendo yao. Pia ameitaka Serikali kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa sheria zinazodhibiti matumizi ya pombe, tumbaku na dawa za kulevya.

Kwa upande wake, mwandishi wa habari John Martin amesema semina zinazotolewa kwa waandishi wa habari zina umuhimu mkubwa katika kuongeza maarifa na kuwawezesha kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, pombe na tumbaku, akisisitiza kuwa elimu haina mwisho.

0/Post a Comment/Comments