Na,
Egidia Vedasto,
Arusha.
Mwaanasheria Mkuu wa Serikali nchini, Hamza S. Johari, amesisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano baina ya taasisi zinazounda UTATU katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, akieleza kuwa kufikiri na kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia kuleta matokeo makubwa na yenye manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Akizungumza Leo Novemba 19,2026katika ufunguzi wa mkutano wa sita wa sita wa Taasisi zinazounda UTATU Jijini Arusha, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya maboresho katika utendaji wa taasisi hizo kwa kuzingatia misingi ya uadilifu, utawala bora na uwajibikaji.
Aidha, amepongeza namna ukaguzi na tathmini za utendaji zinavyofanyika, huku akiunga mkono kuendelezwa kwa mafunzo ya mara kwa mara ya akili mnemba ili kuongeza uwezo wa wataalamu, hususan katika masuala ya upelelezi na ushahidi.
Johari amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika uchunguzi wa makosa ya kifedha na kuhakikisha wahalifu hawapati fursa ya kunufaika na vitendo vyao. Amesema matumizi ya ushahidi wa kisayansi katika uchunguzi na uendeshaji wa mashauri yatasaidia kupunguza malalamiko na kuongeza ufanisi wa utoaji haki.
Vilevile amesisitiza kuwa makundi maalumu yakiwemo watoto, wazee na watu wenye ulemavu yanapaswa kuendelea kupewa kipaumbele na kuzingatiwa katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo, kwa mujibu wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Johari Amehimiza kikao hicho kujadili changamoto na kasoro zilizopo na kuweka maazimio yatakayosaidia kuboresha utendaji. Amehimiza umuhimu wa kuhakikisha michakato ya upelelezi na uendeshaji wa mashitaka inachukua muda mfupi ili kuharakisha upatikanaji wa haki.
"Wachunguzi na waendesha mashitaka washirikiane kwa karibu katika kukamilisha majukumu yao, mazingira na taratibu za kuwakamata watuhumiwa yazingatie sheria na kuheshimu haki za binadamu kama ilivyoelekezwa na Rais" amesema Johari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai, amepongeza ushirikiano na uwajibikaji uliooneshwa na taasisi zinazounda UTATU kwa kusimama imara katika kipindi kigumu ambacho nchi imepitia kabla na baada Oktoba 29, 2025.
Amesema utendaji kazi wenye ufanisi unategemea mshikamano na ushirikiano baina ya taasisi husika, akieleza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu yake yametokana na maboresho makubwa yaliyofanyika katika mfumo wa utoaji haki nchini.
Aidha, amewataka viongozi wa taasisi hizo kuendelea kudumisha ushirikiano na uwajibikaji ili kuimarisha mafanikio yaliyopo na kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinapatiwa ufumbuzi kwa pamoja.
Pia ametoa wito kwa viongozi walioshiriki mkutano huo kuanza maandalizi ya tathmini ya Kikosi Kazi (Task Force) ya mwaka 2028, ambayo itakuwa awamu ya tatu, kufuatia Tanzania kuondolewa rasmi Juni 13, 2025 katika orodha ya nchi zilizokuwa zinatakiwa kufanyiwa tathmini hiyo.
Katika namna hiyo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Sylivester Mwakitau, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya taasisi zinazounda UTATU ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama na kuwa na uwezo wa kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Amesema taasisi hizo zimepewa dhamana ya kutekeleza sheria na kuhakikisha haki za wananchi zinapatikana bila kucheleweshwa, hivyo ni muhimu kuimarisha ushirikiano katika kutekeleza majukumu hayo kwa ufanisi.
Mwakitalu ameeleza kuwa ushirikiano huo unapaswa kuanzia ngazi ya Taifa hadi Wilaya ili kuhakikisha mifumo ya upelelezi, uchunguzi na uendeshaji wa mashauri inafanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki.
"Ni muhimu kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo kuelekea mkutano wa mwaka 2027, ili kubaini mafanikio na maeneo yanayohitaji maboresho kwa lengo la kuhakikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, yanayolenga upatikanaji wa haki kwa usawa, yanafikiwa" amesema Mwakitalu.
Taasisi zinazounda UTATU huo na kuhakikisha haki inapatikana Kwa usawa Kwa Wananchi ni pamoja na Ofisi ya taifa ya mashitaka (NPS), Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya (DCEA)Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (PCCB) pamoja na jeshi la Wananchi. Kaulimbiu ya mkutano huo ni "Ushirikiano wa Wadau Dhidi ya Uharifu; Tanzania Salama Kuelekea Dira 2050".



Post a Comment