MOUNT MERU YATOA HUDUMA BURE KUADHIMISHA MIAKA 100.



Na, 

Egidia Vedasto,

 Arusha.

Kambi ya matibabu bure inaendela katika viwanja vya hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Jijini Arusha. 

Hatua hiyo imekuja kufuatia maadhimisho ya miaka 100 ya tangu huduma zianze kutolewa katika hospitali hiyo 1926, ambapo ilianza kama kituo kidogo cha afya kikitoa huduma za afya Kwa majeruhi waliopogana vita ya kwanza na ya pili.

Akizungumza leo novemba 02,2026 Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Mount Meru Dr. Alex Ernest amewataka Wananchi kuendelea kujitokeza Kwa wingi kupata huduma za vipimo na matibabu ya macho, watoto na magonjwa mengine hadi Novemba 09, 2026 siku moja kabla ya maadhimisho hayo.

 Hata hivyo kampeni ya uchangiaji damu inaendelea viwanjani hapo, Wananchi wameombwa kuendelea kujitokeza Kwa wingi kuchangia damu kufuatia mahitaji makubwa yaliyopo katika hospitali hiyo ambapo zinatakiwa chupa 450-550 Kwa mwezi.




 

0/Post a Comment/Comments